Mahsmbulizi manne yauwa dazeni Burkina Faso

Takriban mashambulizi manne yanayo shukiwa kufanywa na wenye msimamo mkali nchini Burkina Faso, yameuwa dazeni ya wanajeshi na raia katika wiki moja kwa mujibu wa vyanzo vya usalama na kiraia vilivyo zungumza na shirika la habari la AFP, Jumapili.

Vimesema kwamba mashambulizi yalilenga maeneo ya kijeshi toka Jumapili ya wiki iliyopita, na kusababisha vifo vya dazeni za watu wengi kutoka eneo lenye misukosuko la kaskazini mwa nchi.

Chanzo kimoja cha nchini humo kimesema kundi kubwa la magaidi waliokuwa na silaha lilishambulia kambi ya jeshi mjini Nouna kaskazini magharibi mwa nchi siku ya Jumamosi.

Mapigano hayo yalisababisha madhara kwa jeshi na raia. Vyanzo vinasema mashambulizi mengine mawili katika kambi za jeshi yalifanyika Desemba 24.

Kundi la wenye msimamo mkali la GSIM lenye uhusiano na Al-Qaida, limedai kuhusika na mashambulizi hayo na kutangaza kuwauwa wanajeshi 60.