Kimbunga kilipiga Mayotte Katikati mwa Desemba na kusababisha uharibifu mbaya kwenye kisiwa hicho maskini kinachomilikiwa na Ufaransa
Watu 39 waliuawa na zaidi ya 5,600 kujeruhiwa.
Lengo kubwa la ufaransa ni kuunganisha umeme kwa kila boma ifikapo mwishoni mwa January.
Huduma za dharura zinaendelea kujaribu kurejesha maji, umeme na mawasiliano katika kisiwa cha Mayotte, wiki mbili baada ya kutokea kimbunga.
Francois Bayrou aliandamana na Waziri wa elimu Elizabeth Borne Pamoja na Waziri mpya wa kusimamia majimbo ya n’gambo ya Ufaransa Manuel Valls
Mbunge wa mrengo wa kati Estelle Youssouffa, anayewakilisha kisiwa cha Mayotte, amesema mpango wa kutoa msaada wa Ufaransa hautoshi mahitaji ya Mayotte, ikiwemo maelfu ya wahamiaji wasiokuwa na vibali rasmi.