Mahakama ya Ufaransa imewakuta na hatia watu 51 kwa ubakaji

Picha ya Gisèle Pelicot na mume wake wa zamani Dominique Pelicot wakiwa mahakamani siku za nyuma, katika picha iliyochorwa na Valentin Pasquier. France, Sept. 17, 2024.

Dominique Pelicot alikiri kosa la kumlewesha Gisele Pelicot na kumbaka na kuutoa mwili wake bila ridhaa kwa ajili ya ngono

Mahakama ya Ufaransa leo Alhamis imewakuta na hatia ya washtakiwa wote 51 katika kesi ya dawa za kulevya na ubakaji ambayo iliitisha dunia na kumbadilisha muathirika, Gisele Pelicot, kuwa ni ishara ya ujasiri.

Mume wa zamani wa Pelicot wa miaka 50, Dominique Pelicot, alikiri kosa la kumlewesha mara kwa mara kwa takribani muongo mmoja, kwa kumbaka na kuutoa mwili wake bila ridhaa kwa ajili ya ngono kwa wageni kadhaa aliokutana nao mtandaoni, huku video ikirekodi unyanyasaji huo.

Jopo la majaji watano lilimhukumu kifungo cha miaka 20 jela, kama ilivyoombwa na waendesha mashtaka. Mahakama iliweka masharti mafupi zaidi ya miaka minne hadi 18 iliyotakiwa na upande wa mashtaka kwa washtakiwa wengine, ambao karibu wote walishtakiwa kwa kumbaka Gisele Pelicot.

Kwa ujumla, mahakama iliwakuta washtakiwa 47 na hatia ya ubakaji, wawili wakiwa na hatia ya kujaribu kubaka, na wawili walikutwa na hatia ya unyanyasaji wa kingono.