Mahakama ya Rwanda yamuachilia huru mpinzani aliyezuiliwa jela kwa ubakaji

Wafungwa wakisimama nje ya gereza kuu ya Kigali, Rwanda

Mahakama ya Rwanda Jumatano ilimuachilia huru muhadhiri maarufu wa Chuo kikuu ambaye ni mpinzani wa serikali aliyezuiliwa jela kwa miezi 17 kwa madai ya ubakaji.

Christopher Kayumba alikamatwa mwezi Septemba mwaka wa 2021 baada ya madai yaliyotolewa na watu wengi, akiwemo mwanafunzi wake wa zamani, kulingana na ofisi ya Rwanda ya mashtaka ya umma (RIB).

Kayumba, ambaye alianzisha gazeti la mtandaoni liitwalo “ The Chronicles”, aliunda chama cha kisiasa kinachompinga Rais Paul Kagame.

Muda mfupi baada ya hapo, madai ya ubakaji yaliibuka dhidi yake kwenye mitandao ya kijamii na aliyakanusha.

Alikamatwa na kushtakiwa kwa ubakaji na kushiriki ubakaji.

Lakini majaji watatu wa mahakama mjini Kigali walimuondolea mashata yote Jumatano, wakiamua kwamba ushahidi uliotolewa na upande wa wawaendesha mashtaka hautoshi.

“Mahakama haikumpata Kayumba na hatia kuhusu mashtaka yote na imeamuru kuachiliwa kwake mara moja,” mahakama iliamua.

Kayumba, mwenye umri wa miaka 49 hakuwepo mahakamani wakati wa uamuzi huo.