Majaji watano wa Mahakama ya Abuja wamekuwa wakijadiliana kwa miezi kadhaa kesi za vyama vya upinzani vya Peoples Democratic Party (PDP) na Labour Party vinavyodai kwamba uchaguzi uligubikwa na udanganyifu na kasoro.
Madai ya chama cha Labour kwamba kulikuwa na kasoro zilizojitokeza katika mamlaka ya uchaguzi, wizi wa kura na madai kwamba Tinubu hakustahili kugombea, yametupiliwa mbali na mahakama.
Uamuzi kuhusu ombi la chama cha PDP ulikuwa bado ukisubiriwa.
Katika kinyang’anyiro chenye upinzani mkali, gavana wa zamani wa Lagos Tinubu alipata asilimia 37 ya kura katika uchaguzi wa Februari 25, akiwashinda Atiku Abubakar wa PDP na Peter Obi wa chama cha Labour na kupata urais katika taifa hilo lenye watu wengi barani Afrika.
Wanasheria wanasema uamuzi wowote utakaochukuliwa bado utawasilishwa kwenye mahakama ya juu kwa ajili ya uamuzi wa mwisho.