Mahakama ya kijeshi katika eneo tete la mashariki mwa DRC imewahukumu adhabu ya kifo wanajeshi 22 leo Jumatatu kwa “kumkimbia adui” wakati wa mapigano na waasi wa M23, mwanasheria mmoja ameliambia shirika la habari la AFP.
Wanajeshi 16 walihukumiwa kifo katika kesi moja kwenye jimbo la Kivu Kaskazini, na wengine sita katika kesi tofauti, siku chache baada ya wanajeshi 25 kupewa hukumu kama hiyo.
Hukumu hiyo ya hivi karibuni imekuja wakati waasi wa M23, ambao Kinshasha inaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono, wiki iliyopita waliiteka ardhi mpya katika eneo la kaskazini lenye mgogoro ambao umekuwa ukiendelea kwa miaka miwili na nusu katika jimbo la Kivu Kaskazini.
Mahakama ya kijeshi imewahukumu watu 16 katika kesi moja kwenye mahakama ya Kivu Kaskazini. Upande wa mashtaka uliomba siku ya Jumamosi kwamba watu 22 katika kesi hiyo wahukumiwe kifo.