Mahakama ya Algeria Jumapili imemhukumu mwandishi wa habari maarufu Ihsane El Kadi kifungo cha miaka mitatu jela kwa ufadhili wa kigeni kwa biashara yake, katika kesi ambayo imekosolewa na mashirika ya kutetea haki za binadamu.
El Kadi, mmoja wa viongozi wa mwisho wa vyombo vya habari huru katika taifa hilo la Afrika Kaskazini, akiwa mkurugenzi wa tovuti ya habari ya Maghreb Emergent na Radio M, alihukumiwa kifungo cha miaka mitano, miaka miwili kati yake ikiondolewa.
Mahakama ya Algiers pia iliamuru wakati wa hukumu kufutwa kwa kampuni ya Interface Medias, mchapishaji wa majarida mawili ya El Kadi, na kutaifisha mali yake.
Kampuni hiyo pia ilitozwa faini ya dinari milioni 10 sawa na dola 73,500 huku El Kadi mwenyewe akitozwa faini tofauti ya dinari 700,000.
Wakili wake, Abdelghani Badi, aliiambia AFP kuwa atakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.