Mahakama Ubelgiji yawahukumu wawili miaka 20 kwa jaribio la kigaidi

Salah Abdeslam na Sofien Ayari

Mahakama moja nchini Ubelgiji imewahukumu watu wawili kutumikia kifunguo cha miaka 20 waliokutikana na hatia ya jaribio la kigaidi la kumuuwa polisi kuhusiana na shambulizi la bunduki la mwezi Machi 2016 huko Brussels.

Wote wawili waliokutikana na makosa –Salah Abdeslam na Sofien Ayari- hawakuwako mahakamani Jumatatu wakati kesi hiyo inaamuliwa.

Abdeslam yuko jela nchini Ufaransa akisubiri kesi yake kusikilizwa juu ya kushiriki kwake katika shambulizi la kikundi cha Islamic State (IS) huko Paris Novemba 2015.

Waendesha mashtaka wanasema kuwa peke yake ndiye aliyesalimika katika kikundi cha IS ambao walijitoa muhanga.

Juu ya kuwa watu hao wawili walikuwa hawajafika mahakamani, kulikuwa na ulinzi mkali katika eneo hilo la mahakamani nje na ndani ya mahakama.