Mahakama Russia yaongeza muda wa kukaa kizuizini  kabla ya kusikilizwa kesi ya mwanahabari wa Marekani

Picha iliyotolewa na Mahakama ya Jiji la Moscow Machi 26, 2024 inamuonyesha mwandishi wa habari wa Marekani Evan Gershkovich, aliyekamatwa kwa mashtaka ya ujasusi huko Moscow. (Picha na Kitini AFP)

Mahakama moja ya Russia imeongeza muda wa kukaa kizuizini  kabla ya kusikilizwa kesi ya mwanahabari wa Marekani Evan Gershkovich, ambaye alikamatwa karibu mwaka mmoja uliopita kwa tuhuma za ujasusi zinazochukuliwa kwa sehemu kubwa ni uongo

Mahakama hiyo Jumanne iliamuru Gershkovich azuiliwe hadi Juni 30, ikiwa ni kuongeza kwa miezi mitatu amri iliyotolewa awali.

Hakuna tarehe ya kesi yake iliyotajwa.

Gershkovich mwenye umri wa miaka 32 alikamatwa akiwa katika safari ya kuripoti katika mji wa Yeka-terinburg nchini Russia Machi 2023.

Gershkovich na gazeti hilo wamekanusha madai ya ujasusi ya Russia. Lakini Russia haijatoa ushahidi wa mashtaka hayo.