Mahakama moja ya Bangladesh imetoa hati ya kukamatwa Sheikh Hasina

Sheikh Hasina, Waziri Mkuu wa zamani wa Bangladesh

Hasina na watu wengine 45 wakiwemo washauri wake wa karibu wanashtakiwa kwa mashtaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Mahakama moja maalum nchini Bangladesh leo Alhamis imetoa hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa zamani Sheikh Hasina na watu wengine 45, wakiwemo washauri wake wa karibu kwa mashtaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu wakati wa maandamano ya wanafunzi mwezi Julai na Agosti ambayo yalimlazimisha kukimbia nchi.

Mwendesha mashtaka B.M. Sultan Mahmud amesema mahakama ya kimataifa ya uhalifu yenye makao yake Dhaka, chini ya mshindi wa tuzo ya Nobel Muhammad Yunus, kiongozi wa mpito wa nchi hiyo, ilitoa hati ya kukamatwa katika kujibu maombi mawili yaliyowasilishwa na upande wa mashtaka.

Alisema mkuu wa mahakama hiyo, Golam Mortuza Majumdar, alitoa amri hiyo mbele ya majaji wengine. Mahakama hiyo kwanza ilikubali ombi letu ambalo lilimhusisha Sheikh Hasina peke yake.

Kisha tukapeleka ombi letu la pili dhidi ya watu 45 ambao ni wasaidizi wake wa karibu, pamoja na wengine kwa uhalifu dhidi ya binadamu. Pia ombi lilikubaliwa na mahakama, alisema mwendesha mashtaka kwa njia ya simu.