Mahakama moja mjini Kampala imekata maombi mawili yaliyofikishwa mahakamani Jumatatu na mwandishi vitabu mashuhuri wa Uganda na mkosowaji wa serikali Kakwenza Rukirabashaija.
Mwandishi huyo aliyefika mahakamani leo akiwa pamoja na mawakili wake waliomba arudishiwe pasporti yake na aruhusiwe kwenda Kenya kupata matibabu baada ya kuteswa akiwa kizuizini tangu disemba 28.
Uamuzi huo umetolewa wakati Ubalozi wa Umoja wa Ulaya mjini Kampala, ulipotoa tarifa hii leo kutaka waliohusika na vitendo vya kumtesa Rukira-bashaija akiwa kizuizini wahukumkiwe. Tarifa ya EU inasema kwamba inaungana na waganda kueleza hasira zao kutokana na ripoti kwenye vyombo vya habari kwamba mwandishi huyo aliteswa vibaya na maafisa wa usalama waliokua wanamshikilia.
Rukirabashaija alikamatwa kwa kuandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa tweeter unaomkosowa Rais Yoweri Museveni na mtoto wake wa kiume Muhoozi Kainerugaba mwenye ushawishi mkubwa nchini Uganda.