Magufuli azungumzia kuimarisha uhusiano wake na Kenyatta

Rais Uhuru Kenyatta akimkaribisha mwenzake John Magufuli ikulu Nairobi

Rais wa Tanzania John Pombe Mgufuli, siku ya Jumatatu alitetea uhusiano wake na rais Uhuru Kenyatta na kusema kuwa tofauti na tetesi kwamba uhusiano wa kidiplomasia umezorota ni mambo yasio na msingi.

Alisisitiza kwamba wanazungumza kila mara kwa mara kwa njia ya simu juu ya uhusiano kati ya nchi zao na masuala mengine ya kikanda na kimataifa.

Rais Magufuli alifafanua suala hilo la uhusiano alipozungumza na waandishi wa habari akiwa katika ziara yake ya kwanza Kenya tangu kuchukua madaraka mwaka mmoja uliyopita.

Your browser doesn’t support HTML5

Magufuli azungumzia uhusiano wake na Kenyatta

Na BMJ Muriithi