Kati ya waliopewa msamaha ni watu 256 ambao awali walikabiliwa na hukumu ya kifo.
Hatua hiyo ni mwendelezo wa utamaduni wa kuwaachilia wafungwa katika taifa hilo la Afrika Mashariki wakati wa maadhimisho ya siku hiyo muhimu kihistoria.
Jamhuri ya muungano wa Tanzania ilihasisiwa tarehe 26 mwezi Aprili mwaka 1964 Tanganyika kuukngana na Zanzibar.
Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ya Ikulu, Gerson Msigwa, ilieleza kwamba Rais Magufuli ana imani kwamba wafungwa hao wamepata funzo lililokusudiwa na kwamba watajiunga na Watanzania wengine kulijenga taifa.
Magufuli aliwataka Watanzania kuitizama sikukuu ya Muungano kama nafasi nzuri ya kutafakari na kumuomba Mungu kuwaokoa kutokana na janga la Corona, kwa mujibu wa gazeti la The Citizen.