Maelfu ya watu wamehamia katika makazi ya muda katika Kisiwa cha Sumatra, Indonesia, idara ya maafa ya nchi hiyo imesema Alhamisi.
Mvua kubwa zinazo nyesha Kaskazini ya Sumatra wiki hii zilisababisha maafa hayo, na wengi walizama ndani ya maji au kupigwa na magogo ya miti yaliyo kuwa yanapelekwa kwa kasi na mawimbi, shirika hilo limesema.
Wataalam wa mazingira wanaeleza kuwa ukataji haramu wa miti ulokithiri katika kisiwa hicho huwenda umechangia mafuriko hayo kulingana na maafisa wa kiswa bkutokana na momonyoko wa udongo.
Mwezi huu, kipimo kikubwa cha mvua kilisababisha mafuriko na maporomoko yaliyouwa takriban watu 70 ndani na maeneo yanayo izunguka Jakarta, ambayo iko jirani na kisiwa cha Java.
Maeneo ya jirani na mji mkuu wa Indonesia – jiji kuu lenye wakazi zaidi ya watu milioni30 – yalizama katika mafuriko hayo na kuwafanya maelfu ya watu kuishi katika kambi za muda.
Kisiwa kilichoko Kusini mashariki mwa Asia mara kwa mara imekuwa ikikumbwa na mafuriko wakati wa msimu wa mvua, zilizoanza mwisho wa mwezi Novemba.