Mafuriko yahatarisha maisha ya maelfu Russia

Maji ya mafuriko yaliongezeka katika miji miwili ya milima ya Ural, nchini Russia, Jumapili baada ya mto wa tatu ambao ni mrefu sana  barani Ulaya kufurika maji.

Maji hayo yalifika hadi kwenye bwawa, na kusababisha mafuriko ya takriban nyumba 6,000 na kuwalazimu maelfu ya watu kukimbia na mali chache muhimu.

Safu ya mikoa ya Russia, katika Milima ya Ural, na Siberia, kando na maeneo jirani ya Kazakhstan, yamekumbwa na mafuriko katika siku za hivi karibuni na katika miongo kadhaa.

Mto Ural, uliongezeka maji kwa mita kadhaa Ijumaa kutokana na kuyeyuka kwa maji ambayo yanapita kwenye bwawa katika mji wa Orsk, kilomita 1,800 mashariki mwa Moscow.

Zaidi ya watu 4,000 walihamishwa huku maeneo ya jiji lenye watu 230,000 yalifurika.

Picha zilizochapishwa na wizara ya dharura zilionyesha watu wakiwaokoa mbwa waliokwama na kusafiri kwenye barabara zilizofurika kwa boti na mitumbwi.