Mafuriko na maporomoko ya ardhi katika eneo la pwani ya Kenya yamesitisha huduma za usafirishaji mizigo kwa njia ya reli kwenda na kutoka katika mji wa bandari wa Mombasa, shirika la reli la serikali lilisema Jumamosi.
Mvua kubwa ya El Nino, ikifuatiwa na mafuriko makubwa, imefunika miji kote Afrika Mashariki, na kuwaacha maelfu ya watu bila makazi.
Nchini Kenya, idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko ni takriban 46, na inatarajiwa kuongezeka.
Mafuriko na maporomoko ya ardhi kwenye njia ya reli kati ya mji mkuu Nairobi na Mombasa yamelilazimu shirika la reli la Kenya kufunga huduma zote za mizigo, ilisema katika taarifa yake.
Reli hiyo pia husafirisha mizigo katika mataifa mengine katika kanda hiyo, ikiwa ni pamoja na Rwanda, Uganda na Sudan Kusini.