Zaidi ya watu 127,000 wamehamishwa kutoka kaskazini mashariki mwa China kufuatia mafuriko makubwa ambayo yanaripotiwa yemeuwa takriban watu 1,400 mwezi huu.
Shirika rasmi la habari la China Xinhua, liliripoti Jumapili kwamba zaidi ya watu elfu 94 walihamishwa kutoka mji wa Dandong pekee unaopatikana kando ya mto Yalu ulofurika kutokana na mvua nyingi, unaopakana kati ya China na Korea ya Kaskazini.Takriban wakazi elfu tano mia moja wameondolewa kutoka maeneo yaliyoathiriwa huko Korea Kaskazini.
Mvua kubwa tangu Alhamisi zimesababisha mafuriko ambayo yamezomba nyumba karibu kilomita 100 kaskazini mashariki mwa Dandong na kuuwa watu wanne. Watabiri wa hali ya hewa wameonya kwamba kutakuwepo na hadi sentimita 25 za mvua zaidi mnamo masaa 24 ijayo katika eneo hilo.
Matukio mbali mbali yanayotokana na mafuriko huko China mwaka huu yamesababisha vifo vya takriban watu 4,000. Maafisa wa huduma za dharura wa China wanasema idadi ya walofariki kutokana na momonyoko mkubwa wa ardhi mapema mwezi huu katika wilaya ya Zaouqou, kaskaizni magharibi ya nchi imefikia watu 1,434 walofariki na wengine 331 hawajapatikana baado.