“Idadi ya waliofariki ni kubwa,” amesema Tamer Ramadan, mkuu wa ujumbe wa IFRC nchini Libya.
Ramadan amesema shirika lake limethibitisha kutoka vyanzo huru kwamba kuna watu 10,000 hawajulikani walipo.
Maafisa mashariki mwa Libya walisema Jumatatu kwamba takriban watu 2,000 wanaaminaka walifariki katika mji wa Derna.
Eneo hilo lilikumbwa na mvua kubwa na mafuriko kutokana na kimbunga Daniel kutoka Mediterranean, na kusababisha mabwawa kupasuka na vitongoji vyote kusombwa na maji.
Video iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii ilionyesha mitaa imegeuka mito iliyofurika katika miji ya Derna pamoja na Benghazi, Sousse, Al Bayda na Al-Marj.