Maelfu ya Wamarekani wanaotumia TikTok wajianda kuhamia kwenye mitandao mingine ya kijamii

  • VOA News

Picha hii inayoonyesha nembo ya TikTok mbele ya bendera za Marekani na China. Picha ya AFP

Huku muda wa mwisho wa Jumapili ukikaribia kwa Tiktok kutafuta mmiliki mwingine au kukabiliwa na vikwazo vya Marekani, maelfu ya Wamarekani wanaotumia mtandao huo maarufu wa kijamii wanasema wanahamia kwenye program nyingine ya mtandao wa kijamii wa China, Xiaohongshu au RedNote.

Baadhi wanasema wanachukua hatua hiyo, wakijiita “Wakimbizi wa TikTok” kwa kutafuta makazi mapya, wengine wanasema kuhama kwao ni njia ya kupinga marufuku dhidi ya TikTok.

Huku zikiwa zimesalia siku chache kabla ya muda wa mwisho, wanaotumia mtandao huo wanakabiliwa na hali ya sintofahamu inayozidi kuongezeka, huku wakisubiri uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Marekani iwapo au la itaidhinisha marufuku hiyo.

Ripoti sasa zinabashiri kwamba TikTok inaweza kufunga shughuli zake nchini Marekani ikiwa marufuku hiyo itapitishwa.