Maafisa wa Palestina wanasema mtu mmoja ameuawa na wengine wanne kujeruhiwa vibaya. Mauaji hayo ya risasi, yalifuatiwa na shambulio la usiku wa manane, yanaibua maswali kuhusu tamko la Jordan kwamba ilipokea uhakikisho kutoka kwa waisrael na Wapalestina kutuliza wimbi la ghasia lililodumu kwa mwaka mzima.
Vurugu hizo zilitokea muda mfupi baada ya serikali ya Jordan, ambayo ilikuwa mwenyeji wa mazungumzo ya Jumapili kwenye eneo la mapumziko la Bahari ya Sham la Aqaba, kusema pande zote zimekubaliana kuchukua hatua za kupunguza mivutano na zitakutana tena mwezi ujao kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa waislamu.