Eneo la Plaza kawaida linaaminika kupokea karibu watu 100,000, lakini waandamanaji wengi ambao hawakuweza kuingia katika eneo hilo walikusanyika kwenye mitaa ya karibu na eneo hilo.
Waandamanaji wengi walikuwa wamevalia mavazi ya rangi ya taasisi ya kitaifa ya uchaguzi, wakipaza sauti na kusema “ Usibadili kura yangu”.
Madabiliko ya sheria ya uchaguzi yamepelekea Marekani kueleza msimamo wake.
Brian A. Nichols, waziri mdogo wa Marekani anayehusika na masuala ya kanda ya magharibi, ameandika kwenye Twitter “Leo huko Mexico, tunashuhudia mjadala mkubwa kuhusu mageuzi ya uchaguzi ambayo ni mtihani kwa uhuru wa taasisi za uchaguzi na mahakama.”
“Marekani inaunga mkono taasisi huru za uchaguzi zenye uwezo wa kutosha ambazo zinaimarisha michakato ya kidemokrasia na utawala wa sheria,” Nichols aliandika.
Mapendekezo ya Rais Obrador yalipitishwa wiki iliyopita. Ikiwa yataanza kutekelezwa, yatapunguza mishahara, fedha za ofisi za uchaguzi wa mitaa na mafunzo kwa waninchi wanaofuatilia na kusimamia uchaguzi kwenye vituo vya kupigia kura. Yatapunguza pia adhabu kwa wagombea wanaoshindwa kuripoti matumizi ya kampeni zao za uchaguzi.