Taarifa ilidai manyanyaso kwa wapiga kura, rushwa, kuonyesha kinyume cha sheria vifaa vya kampeni kwenye vituo vya kura, kuwadughudhi mawakala wa chama na matumizi yasiyo sahihi ya vifaa vya uchaguzi. Haikutoa ushahidi na haikuelezea kwanini shutuma hizo zilitolewa kwa kuchelewa. Maafisa wa vyaa hawakuweza kufikiwa kutoa maoni yao.
Kama maafisa wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) wanavyofafanua na kutoa hesabu ya matokeo, vituo vya televisheni nchini Kenya vimekuwa vikitoa hesabu zao wenyewe, kulingana na fomu, lakini waliacha kufanya hivyo siku ya Alhamisi, huku kukiwa na takriban kura milioni moja zikiwa zimebaki kuhesabiwa.
Watendaji wakuu kutoka mashirika ya Citizen na Nation walisema wafanyakazi wao wamechoka na walihitaji kupumzika.
“Hivi sasa tuna kiasi cha theluthi moja ya watu wanaofanya kazi ambao tulianza nao na tuna azma ya kuendeleza kasi hiyo katika saa chache zijazo wakati timu nzima itakaporejea,” alisema Linus KaiKai, Mkurugenzi wa Mkakati wa Citizen..
Stephen Gitagama, mtendaji mkuu wa Nation Media Group, alisema wafanyakazi wake pia walihitaji mapumzikona kwamba wao wanalenga katika ubora. Aliitaka Reuters waende kwenye tume ya uchaguzi IEBC.
“IEBC ina wajibu wa kutoa matokeo, na siyo vyombo vya habari,” alisema.
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati aliwasihi wakenya kutokuwa na wasi wasi kuhusu matokeo tofauti yaliyotabiriwa na vituo mbali mbali vya televisheni.
“Hakuna haja ya kuwa na wasi wasi kuhus tofauti hizo ambazo tunaziona kwenye televisheni za vyombo vya habari,” alisema, akiongezea kwamba matokeo rasmi huenda yatakatolewa na IEBC, ambapo itayachapisha matokeo Agosti 16.
Ijumaa asubuhi, tume ya uchaguzi hatimaye ilianza kuonyesha hesbu ya matokeo ya urais kwenye ktuo chake kikuu cha kutangaza matokeo. Imetoa hesabu ya 1.5% ya kura.
Hesabu ya vyombo vya habari, ambao waliacha kutangaza Ijumaa asubuhi, ilionyesha kuwa wagombea wawili wa juu wamekabana vikali, wakiwa chini ya 50% ya kura zinazohitajika kushinda. Chini ya asilimia moja ambayo tu ambayo inawagawanya kati ya wagombea hao wawili.
Zaidi ya 99.7% ya matokeo ya vituo vya kupiga kura yamepatikana lakinimaelfu bado ya kura bado hazijahesabiwa na vyombo vya habari. Kasi ilipungua ghafla katika 80% ya kura zilizokuwa zimehesabiwa.
Kama hakuna mgombea atakeshindwa 50% na kuwa moja, wagombea wawili wa juu wataingia katika duru ya pili.
Upigaji kura wa Jumanne kwa kiasi kikubwa ulikuwa wa amani lakini mizozo ya awali kuhusu uchaguzi wa urais ilifuatiwa na ghasia mbaya sana, na kuleta wasi wasi mkubwa wakati wa matokeo haya ya awali katika kinyang’anyiro cha karibu sana kati ya wagombea wawili wa juu Ruto na Raila Odinga.
Lakini mchakato wa kuthibitisha na hesabu ya kura ulitarajiwa kuchukua siku kadhaa, mitandao ya kijamii ilikuwa imejaa habari potofu kuhusu matokeo, huku wana kampeni wa haki na makundi ya jamii za kiraia yakishutumu kambi za wagombea wote wawili kwa kushirikiana habari ambazo si za kweli.
Hakuna matokeo ya k uraya urais ambayo yalitolewa bila ya kupata ushindani nchini Kenya tangu mwaka 2002, na mizozo ilipelekea umwagaji damu katika siku zilizopita, ama ikihusisha mapambano ya kikabila au ghasia za polisi.
Baada ya uchaguzi war ais wa mwaka 2017 kubatilishwa na Mahakama ya Juu, wakielezea dosari na utawala mbaya uliofanywa na IEBC, tume hiyo ya uchaguzi iko kwenye shinikizo kufanya upigaji kura uwe wa wazi na kuweka fomu kwenye mtandao wake ambazo zinaonyesha matokeo kutoka kila kituo cha kupigia kura.
Ripoti hii imeandaliwa kwa habari kutoka Reuters na Shirika la Habari la Ufaransa (AFP)