Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Jumanne ameitembelea Israel akipeleka ujumbe wa mshikamano na Israel kufuatia shambulio baya la Hamas lakini pia akishinikiza ulinzi wa raia wa Palestina huko Ukanda wa Gaza.
Macron amemwambia Rais wa Israel Isaac Herzog kwamba kilichotokea “haikotosahaulika kamwe” na kwamba kipaumbele cha kwanza ni kuachiliwa huru mateka wote wanaoshikiliwa na Hamas.
“Nataka muelewe kwamba hamko peke yenu katika vita hivi dhidi ya ugaidi,” Macron amesema.
Jeshi la Israel leo limesema liliendesha mashambulizi ya anga huko Gaza, ikiwemo kulenga makao makuu ya operesheni za Hamas na kuua manaibu kamanda kadhaa wa kundi hilo.