Shirika hilo la IOM pia limetahadharisha uwezekano wa hali hiyo ya chuki dhidi ya wahamiaji (xenophobia) kuongezeka iwapo kiini cha sababu zinazopelekea uvunjifu huo wa amani hazita tafutiwa ufumbuzi.
Mwandishi wa VOA ameripoti kuwa IOM imelaani wimbi la vitendo vya chuki venye kuvunja amani vinavyoendeshwa na wananchi binafsi na vyama vya jumuiya katika mji wa Rosettenville, kusini mwa Johannesburg na katika mji mkuu wa Afrika Kusini, Pretoria.
Shirika hilo limetaka serikali ichukue hatua kuleta utulivu na kusitishwa kwa vurugu dhidi ya wananchi wa kigeni, na kuzuia wizi na kuchomwa kwa mali zinazomilikiwa na raia wa kigeni yalioanza kutokea mapema wiki hii.
Waandamanaji Afrika Kusini wana washutumu wahamiaji wa Kiafrika kwa kuwanyang'anya kazi zao na kuhusika na ongezeko la uhalifu.
Msemaji wa IOM, Itayi Viriri amesema wale ambao wana dukuduku dhidi ya wahamiaji hawatakiwi kuchukua sheria mikononi mwao. Wanatakiwa kupeleka malalamiko yao katika vyombo vya serikali.