Mabalozi wa Ulaya wako Tripoli kuiunga mkono serikali mpya ya Libya

Fayez al-Sarraj akiwasili Tripoli, Libya March 30, 2016.

Mabalozi wa Spain, Uingereza na Ufaransa wako Tripoli katika kuunga mkono serikali mpya iliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa.

Ni ziara ya kwanza ya mabalozi kutembelea mji mkuu wa Libya katika miaka miwili baada ya balozi nyingi kufungwa 2014 kutokana na mapigano ya makundi ya wanamgambo. Baadaye Libya iliingia kwenye mapigano ambayo yaliigawanya nchini kati ya serikali mbili zinazopingana na mabunge.

Mabalozi hao baadaye watakutana manaibu wa waziri mkuu mpya, Fayez al-Sarraj.