Uchaguzi wa Marekani
Ushindi mkubwa wa chama cha Republican wakati wa uchaguzi wa kati kati ya mhula siku ya Jumanne huwenda ikamsababisha Rais Barack Obama kutoweza kuendelea na ajenda yake mnamo miaka miwili iliyobaki akiwa madarakani.
Moja wapo ya wabunge wepya wa chama cha Republicans Rand Paul anaeungwa mkono na vuguvugu la Tea Party anasema wapiga kura wa jimbo lake la kusini la Kentucky wamepeleka ujumbe wa wazi kabisa kwamba hawaridhishwi na jinsi Rais Obama anaongoza serikali.
Anasema, "ni ujumbe kutoka watu wa Kentucky, Ujumbe wenye sauti kubwa na wazi unaosema , Tumekuja kuchukua tena serikali yetu."
Wakichukua udhibiti wa Baraza la Wawakilishi na kuongeza viti katika Baraza la Senet, Warepublicans watamwekea upinzani mkubwa Rais obama na mipango yake. Miongoni mwa mipango hiyo ni mageuzi ya mfumo wa uhamiaji wa Marekani, pamoja na sera za nishati.
Viongozi wa republicans wameahidi kujaribu kufutilia mbali sheria mpya ya bima ya afya ambayo Bw Obama alitumia muda mrefu mwaka jana na kazi kubwa kuipitisha.
Mbali na uchaguzi wa kupigania viti vyote 435 vya baraza la wawakilishi kuna viti 37 vya baraza la Senet vinavyogombaniwa na mabaraza kadhaa ya majimbo na serikali za mitaa, na katika mashindano hayo yote inaonekana wa Republicans watapata ushindi.