Maandamano ya wakristo - Damascus

Wakristo nchini Syria wakiandamana mjini Damascus Desemba 24 2024 . Picha: AFP

Mamia ya wakristo wameandamana katika mji mkuu wa Syria wa Damascus, baada ya mti wa krisimasi kuchomwa moto katika wilaya ya al-Suqaylabiyah, mjini Hama, kaskazini mwa nchi hiyo.

Wakristo waliandamana wakibeba misalaba iliyotengenezwa kwa mbao na kupaaza sauti na kutoa ujumbe kwa lugha ya kiarabu unaosema kwamba wao ni wanajeshi wa Yesu, na kwamba kwa damu na roho, watajitolewa kwa niaba ya Yesu.

Maandamano yanajiri wakati kuna ongezeko la mashambulizi dhidi ya sehemu za kuabudu za wakaristo.

Watu wasio julikana wakiwa na bunduki walifyatua risasi Desemba 18, dhidi ya kanisa la Orthodox mjini Hama. walijaribu pia kuharibu msalaba uliowekwa mbele ya kanisa hilo na makaburi.

Viongozi wa kanisa nchini Syria wamewashauri wakristo kupunguza sherehe za krisimasi mwaka huu, licha ya ahadi kutoka kwa kwa viongozi wepya wenye kufuata itikadi kali za kislamu wa nchi hiyo kwamba kila mtu ana uhuru wa kuabudu kulingana na dini yake.