Maandamano ya kupinga sensa Mauritania mtu mmoja auwawa na watu weusi wadai kubaguliwa katika hatua hiyo.
Mtu mmoja aliuwawa huko Kusini mwa Mauritania na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati Polisi walipojaribu kutawanya maandamano ya kupinga sensa ya serikali ambayo wapinzani wanasema inabagua watu weusi.
Maafisa na waandamanaji walisema jana kuwa Polisi walifyatua risasi za moto kwenye kundi la waandamanaji katika mji wa Maghama.
Wamauritania weusi wamepinga sana juhudi hizi mpya za sensa na kufanya maandamano nchi nzima katika wiki za karibuni. Wamesema masharti yao ya kuthibitisha uraia ni magumu sana kwao kuliko wamauritania wenye asili ya kiarabu na sensa hiyo imelenga kuwabagua .