Wafanyakazi, wanaharakati na watu wengine katika nchi za Asia wamejitokeza katika miji mikuu ya Asia na Ulaya kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani huku maandamano yakishuhudiwa kulalamikia ongezeko la chakula na sera za ajira za serikali.
Wanataka haki za kikazi kuimarishwa.
Siku ya wafanyakazi inaadhimishwa na nchi nyingi duniani kuangazia haki za wafanyakazi.
Siku hiyo pia hutumika kuangazia maslahi ya kiuchumi ya wafanyakazi pamoja nay a kisiasa.
Mjini Istanbul, Uturuki, polisi wamewakamata darzeni ya watu waliojaribu kuingia katikati mwa bustan ya Taksim, licha ya amri ya serikali kupiha marufuku maadhimisho ya siku ya wafanyakazi.
Serikali ya rais Recep Tayyio Erdogan, imepiga marufuku mikutano katika bustan ya Taksim kwa sababu za kiusalama lakini baadhi ya vyama vya siasa na miungano ya wafanyakazi wameapa kuingia katika bustan hiyo ambayo ina umuhimu mkubwa kwa vyama vya wafanyakazi.