Maandamano nchini Russia

Waandamanaji mjini Moscow Jumamosi Desemba 24, 2011

Zaidi ya waandamanaji laki moja wajitokeza mjini Moscow Jumamosi

Maelfu ya waandamanaji walikusanyika katika mji mkuu wa Moscow nchini Russia leo Jumamosi, kupinga kile walichodai ni wizi wa kura katika uchaguzi wa bunge uliomalizika majuzi. Polisi mjini humo walisema kuwa watu wapatao elfu 28 walihudhuria maandamano hayo katika mtaa wa Sakharov, ingawa mashahidi wanasema idadi hiyo ilikuwa zaidi ya laki moja. Maelfu ya waandamanaji walikusanyika katika miji mingine ya Russia wiki mbili zilizopita baada ya chama cha Waziri Mkuu Vladmir Putin United Russia party kutangazwa kuwa mshindi ya uchaguzi huo wa Desemba 4. Chama hicho kimekanusha madai hayo.Viongozi wa chama hicho wanapendekeza mabadiliko kadha ya kisiasa ili kuzima sauti ya wapinzani wake mojawapo ikiwa kukubalia magavana kuchaguliwa moja kwa moja ingawa lazima waidhinishwe na Kremlin.