Hatua hiyo ni kutokana na kile walichosema ni ubadhirifu wa mali ya umma, ikichukuliwa dhidi ya mkuu wa utwala Nathaniel McGill, mwendesha mashitaka mkuu Sayma Syrenius Cephus na Bill Twehway ambaye ni mkuu wa idara ya kitaifa ya bandari.
Naibu waziri wa fedha anayeshugulika na maswala ya ugaidi na ujasusi wa kifedha hapa Marekani, Brian Nelson amesema kwamba maafisa hao wamehujumu demokrasia ya Liberia kupitia ufisadi ili wajinufaishe wenyewe. Nelson ameongeza kusema kwamba hatua hiyo ni ushahidi tosha kwamba Marekani itaendelea kuunga mkono watu wa Liberia wakati ikihakikisha kwamba wanaojihusisha na visa vya ufisadi wanawajibishwa.
Kwa mujibu wa vikwazo vilivyowekwa, mali zote za maafisa hao zilizopo Marekani zitashikiliwa na kuripotiwa kwa wizara ya fedha, wakati wale walioshirikiana nao wakiwa kwenye hatari ya kuwekewa vikwazo pia, taarifa imeongeza.