Maafisa waandamizi kutoka zaidi ya darzeni za nchi washiriki katika mazungumzo ya BRICS Afrika Kusini

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa BRICS wakiwa Cape Town, Afrika Kusini

Maafisa wa juu kutoka zaidi ya dazeni za nchi ikiwemo Saudi Arabia na Iran wako katika mazungumzo leo Ijumaa kuhusu uhusiano wa karibu na jumuiya ya nchi za BRICS zenye uchumi unaonyayukia, wakati zikitaka kuimarisha ushirikiano na kujiweka kama hali ya kukabiliana na  nchi za magharibi.

BRICS ambayo sasa inajumuisha Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini inafikiria kupanua uanachama wake kwa nchi nyingi hasa kutoka ukanda wa kusini mwa dunia ambazo zimeonyesha nia ya kujiunga.

Kuna wakati umoja huo ulionekana kama moja ya muungano wenye nchi zenye cuhumi unaonyanyukia, BRICS imechukua sura thabiti zaidi ikisukumwa katika miaka ya karibuni kuwa na muonekano madhubuti zaidi, hasa tangu kuzuka vita vya ukraine February 2022 ikiwa na shinikizo kutoka Russia.

Katika hotuba ya ufunguzi wa majadiliano , mwenyeji Waziri wa Mambo ya Nje Afrika Kusini Naledi Pandor alizungumzia jumuiya hiyo kuwa ni bingwa katika maendeleo duniani.

Alisema ilitelekezwa na mataifa yenye utajiri na taasisi za kidunia wakati wa janga la COVID-19. Iran , Saudi arabia, umoja wa falme za kiarabu, DRC, Comoro , Gabon na kazakhstan zote zilituma wawakilishi Cape Town kwa kile kinachoitwa mazungumzo ya “ Friends of Brics” program rasmi ilionyesha.