Vyombo vya habari vya Uturuki vimesema kuwa polisi wamewakamata washukiwa 13 kutokana na mashambulizi matatu ya kujitoa muhanga yaliotokea Jumanne kwenye uwanja wa ndege mjini Istanbul na kuuwa watu 42 huku wengine 239 wakijeruhiwa.
Ukamataji huo umetokea baada ya msako kwenye maeneo 16 mjini humo ikisemekana kuwa watatu kati ya washukiwa hao ni raiya wa kigeni.
Chombo cha habari kinchomilikiwa na serikali cha Anadolu kimesema kuwa watu wengine 9 wamekamtwa kwenye mji wa bandari ya magharibi wa Izmir wakishukiwa kuwa na uhusiano na kundi la Islamic State nchini Syria kwa njia ya kutoa misaada ya kifedha, mafunzo na mipango ya kiufundi.
Maafisa wa Uturuki wanalaumu kundi la Islamic State kwa mashambulizi hayo ingawa kundi hilo halijasema chochote.