Maafisa hao wamekamatwa katika kaunti za Homabay, Kisumu na Bungoma.
Maafisa wengine wanne wa tume hiyo ya uchaguzi wamesimamishwa kazi katika maeneo bunge ya Ndiwa na Webuye mashariki.
Walikuwa wamekutana kwa siri na wagombea wa kiti cha wawakilishi wa bunge la kaunti, na wagombea wa ubunge.
Kukamatwa kwao kulifuatia taarifa za wananchi, ambao waliwapeleka kwa polisi.
Ushahidi wa video uliotolewa kwa polisi, unaonyesha kwamba katika mojawapo ya tukio, naibu wa msimamizi wa kituo cha kupigia kura alikuwa akimshawishi mkubwa wake kukubali “kumsaidia mmoja wa wagombea kupata ushindi.”
Baadhi ya maafisa wengine wa tume ya uchaguzi katika kaunti ya Bungoma wametoroka baada ya wenzao kukamatwa nyumbani kwa mmoja wa wagombea. Mshukiwa aliyekamatwa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Webuye.