Maafisa wa Israel wamesema mateka 14 wa Israel na wafungwa 42 wa Kipalestina watabadilishana siku ya Jumamosi, huku usitishaji vita wa siku nne ambao ulianza kutekelezwa Ijumaa kati ya Israel na Hamas huko Gaza ukionekana kushika kasi.
Katika kipindi cha kusitisha mapigano, Hamas inataka kuwaachilia huru mateka 50, na Israel wafungwa wa Kipalestina 150 kama sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa wakati wa mazungumzo yaliyoihusisha Israel, makundi ya wapiganaji wa Palestina, Qatar, Misri na Marekani
Pia Jumamosi, London inajiandaa kwa maandamano ya kuiunga mkono Palestina huku maelfu ya watu wakitarajiwa kuhudhuria. Zaidi ya polisi 1,500 wameitwa kazini kwa ajili ya Kampeni ya Mshikamano kwa Palestina. Waandamanaji wamepanga kutembea kutoka Park Lane hadi Whiteh.