Maafisa wa ICC wafika Guinea kuangalia maandalizi ya kesi ya mauaji ya 2009

Kiongozi wa zamani wa Guinea Moussa "Dadis" Camara.

Maafisa wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC ) wamewasili nchini Guinea kufuatilia maandalizi ya kesi iliyo-cheleweshwa kwa kipindi kirefu ya mauaji ya watu zaidi ya 150.

Hapo Septemba 2009, vikosi vilivyo chini wa kiongozi wa zamani wa serekali ya mapinduzi Moussa Dadis Camara, vilifyatua risasi kwa wafuasi wa upinzani waliokuwa wakiandamana katika uwanja katika mji mkuu wa taifa hilo la Afrika magharibi Conakry.

Takriban watu 157 waliuwawa, huku wanawake 109 wakibakwa.

Uchunguzi uliokamilishwa 2017, umewatambua dazeni ya washukiwa ikijumuisha kongozi wao Camara.

Lakini licha ya ahadi za rais aliyechaguliwa kuchukuwa nafasi ya Camara, Alpha Conde, kesi hiyo imekuwa ikicheleweshwa na kuzua ukosoaji mkubwa kutoka kwa watetezi wa haki za binadamu.

Serekali ya kimapinduzi ambayo ilimuondoa rais Conde, madarakani, imetoa amri ya kuanza kwa kesi hiyo kabla ya maadhimisho ya mauaji hayo ya 13 itakapofika Septemba 28, licha ya tarehe kutotangazwa.

Maafisa wa ICC ikijumuisha naibu mwendesha mashitaka mkuu Mame Mandiaye Niang, waliwasili Jumatatu usiku.

Niang amesema ziara yao ilifanikishwa na maelekezo ya kiongozi wa mapinduzi Mamady Doubouya, kwa waziri wake wa sheria kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo kabla ya maadhimisho ya tukio hilo.

Wakati wa ziara hiyo maafisa wa ICC watakutana na mamlaka za kisheria za Guinea, na makundi ya walio athirika kimesema chanzo cha mamlaka za kisheria za Guinea.