Maafisa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo watakuwa wakielekea nyumbani kutoka kwenye mkutano wa siku mbili wa ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) mjini Beijing huku wakiwa wamepata mafanikio madogo katika juhudi zao za kupanua uhusiano wa kiuchumi, zaidi ya mauzo ya madini ambayo yametawala biashara, wachambuzi wanasema.
China itaendelea kutaka kuimarisha msimamo wao nchini Kongo, ikijumuisha kwenye madini, anasema Jean-Pierre Okenda, mshauri wa Kongo kuhusu masuala ya madini.
Ingawa DRC inafanya biashara kubwa ya madini na China, wakati nchi nyingi za Afrika zina madeni makubwa, karibu yote ni kutoka kwa madini ambayo China inanunua kuwapatia wazalishaji wake ambao wanahitaji sana malighafi.
Taifa hilo la Afrika ya kati, ndiyo mzalishaji mkubwa zaidi wa shaba na kobalti duniani, mali ghafi inayotumika katika vifaa vya elektroniki, na nyenzo muhimu kwa betri zinazotumika katika magari ya umeme. DRC ina asilimia 70 ya akiba ya Kobalti