Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia Alhamisi ilitangaza kupigwa marufuku kwa watu saba ambao ni wanafanya kazi kwa mashirika yasiyo ya serikali ndani ya nchi hiyo kwa shutuma za kuingilia mambo ya ndani ya taifa hilo.
Kulingana na barua zilizopelekewa kila mmoja wa watu 7, wote wamepewa saa 72 kuondoka nchini Ethiopia.
Wafuatao ndio walioamriwa kuondoka:
1. Adele Khodr, mwakilishi wa UNICEF nchini Ethiopia
2. Sonny Onyegbula,UNHCR
3. Kwesi Sansculotte, UNOCHA
4. Saeed Mohamoud Hersi: Afisi ya uratibu wa misaada Ethiopia.
5. Grant Leaity, Afisa wa masuala ya huduma za binadamu Ethiopia
6. Bi Ghada Eltahir Mudawi: Afisa wa masuala ya huduma za binadamu Ethiopia
7. Bi Marcy Vigoda, Afisa wa masuala ya huduma za binadamu Ethiopia
Habari zaidi zitafuata...