Desemba Mosi inaadhimishwa siku ya ukimwi duniani kote. Lakini miaka mitano iliyopita kulikuwa hakuna madawa mahsusi ya kuwasaidia watoto wanoishi na virusi vya HIV na Ukimwi. Vipimo vya dawa kwa watu wazima ndivyo vilivyopunguzwa na kupewa watoto, mara nyingi zikiwa na madhara makubwa kwa watoto. Wakati mwingine watoto walipewa madawa mengi yenye ladha mbaya. Lakini Kufuatia juhudi za kimatiafa makampuni ya kutengeneza madawa yametengeneza dawa za kudhibiti HIV na Ukimwi kwa watoto ambazo zina ladha inayokubalika kwao . Huko nchini Kenya watoto mayatima wa Ukimwi wanaoishi kwenye makazi ya hifadhi ya watoto inayoitwa NYUMBANI mjini Nairobi, dawa hizo maalum kwa watoto zinakaribishwa. Kwa maisha yake mafupi, Lazarus mwenye umri wa miaka 14, amekuwa katika mpangilio maalum wa dawa anazosema ni rahisi na ngumu kutumia. Anasema akimeza dawa hizi asubuhi ni rahisi, lakini baadaye ni ngumu. Asubuhi anameza tembe nne za dawa, na jioni tembe sita. Na akizitumia hizo dawa za jioni anapata kizunzi na kuumia shingoni. Hali ya Lazarus inamulika kile ambacho watoto wanoishi na HIV na ukimwi hupitia wanapopata matibabu. Mara nyingi inawabidi wachukuwe dawa nyingi na chungu. Pia mara nyingi dozi za dawa za watu wazima hugawanywa vipande wakapewa watoto, jambo ambalo ni hatari iwapo dawa hizo hazikuvunjwa sawasawa. Lakini mwishoni mwa mwaka 2006, UNITAD, mradi wa ulimwengu wa afya uloanzishwa na nchi tano, Brazil, Ufaransa, Norway, Chile na Uingereza kuongeza upatikanaji wa dawa katika nchi zinazoendelea, ilianza mradi wa kutengeneza ,dawa ya kudhibiti ukimwi ambayo yana ladha inayoweza kuvutia watoto.
Msemaji wa UNITAD Daniela Bagozzi anaeleza kwamba katika nchi zilizoendelea hakuna watoto wanozaliwa na HIV kwa vile hatuwa zimechukuliwa kuzuwiya usambazaji wa HIV wakati wa uja uzito. Katika nchi zinazoendela, UNITAD inakadiria kwamba kuna takriban watoto millioni 2 na nusu wanoishi na HIV, tisa kati ya kumi wako barani Afrika katika nchi chini ya jangwa la sahara.