M23 yachukuwa udhibiti wa Matembe

Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo limepoteza eneo Jumatatu katika mapigano na waasi wanaoungwa mkono na Rwanda mashariki mwa nchi, duru za kijeshi na za ndani zinasema, siku moja baada ya mkutano wa amani kati ya marais wa nchi hizo mbili kufutwa.

Toka 2021, wanamgambo wa waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Kigali wameteka maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kusababisha maelfu ya watu kuhama makazi yao na kusababisha mzozo wa kibinadamu.

Vikosi vya jeshi la DRC vilipoteza udhibiti wa Matembe, mji katika jimbo la Kivu Kaskazini ulioko kwenye barabara inayoelekea kituo kikuu cha biashara cha Butembo, baada ya mapigano kuzuka Jumapili na M23, kwa mujibu wa vyanzo vya ndani na kijeshi.

Mapigano yalianza Jumatatu katika vilima vya Matembe na mji jirani wa Vutsorovya, msemaji wa washirika wa Kinshasa wanaoendesha shughuli zao sambamba na jeshi katika eneo hilo, ameiambia AFP.