Aliyekuwa mgombea urais nchini Tanzania, kwa tikiti ya chama cha upinzani, Chadema, Tundu Lissu, amemkosoa rais wa nchi hiyo John Magufuli, kwa jinsi anavyolishughulikia suala la janga la Corona.
Lissu amesema kuwa, iwapo utawala wa Rais Magufuli hautabadilisha msimamo uliouchukuakua kuhusu maambukizi ya virusi hivyo, basi Watanzania wataendelea kupoteza maisha yao, jambo ambalo, amesema, ni la kutia wasiwasi mno.
Lissu, ambaye yuko nchini Ubelgiji, alikuwa akizungumza na BMJ Muriithi ambaye hapa anaanza kwa kueleza mtazamo wake kuhusu hali ya Covid-19 nchini Tanzania.
Your browser doesn’t support HTML5
Tazama kwa mtandao wa Youtube:
https://www.youtube.com/watch?v=lZFAlQpd7hk&feature=youtu.be