Lionel Messi ashinda Balon d’Or kwa mara ya saba

Mchezaji wa Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi akifurahi baada ya kupata tuzo ya Ballon d'Or 2021 iliyotolewa na France Football huko Theatre du Chatelet mjini Paris November 29, 2021. (Picha na FRANCK FIFE / AFP)

Mchezaji wa kimataifa wa PSG na Argentina Lionel Messi ameshinda tena Ballon d'Or kwa upande wa wanaume kwa mara ya saba usiku wa Jumatatu akimaliza mwaka kwa mtindo baada ya msimu mzuri wa mwisho akiwa na Barcelona na kutwaa taji lake la kwanza kuu la kimataifa na timu yake ya taifa ya Argentina.

Mchezaji wa kimataifa wa PSG na Argentina Lionel Messi ameshinda tena Ballon d'Or kwa upande wa wanaume kwa mara ya saba usiku wa Jumatatu akimaliza mwaka kwa mtindo baada ya msimu mzuri wa mwisho akiwa na Barcelona na kutwaa taji lake la kwanza kuu la kimataifa akiwa na timu yake ya taifa ya Argentina.

Alexia Putellas alikua mshindi wa tatu wa tuzo hiyo kwa upande wa wanawake kwa msimu bora na timu yake ya Barcelona na Uhispania.

Messi mwenye umri wa miaka 34 aliiongoza Argentina kutwaa taji la Copa America mwezi Julai baada ya kushindwa katika fainali nne kuu za kimataifa.

"Nina furaha sana kuwa hapa, nina furaha kuendelea kupigania mataji mapya," alisema kupitia mkalimani. "Sijui ni miaka mingapi iliyobaki, lakini natumai mingine mingi. Ningependa kuwashukuru wachezaji wenzangu wote (wa zamani) Barcelona na Argentina."

Messi alimaliza akiwa na pointi 613 kileleni mwa mshambuliaji mahiri wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski akiwa na pointi 580.

"Ningependa kumwambia Robert kwamba ni heshima kuwa mpinzani wako, na kila mtu angesema ulistahili kushinda mwaka jana," Messi alisema.

Ikitolewa na jarida la France Football, Ballon d’Or imekuwa ikitolewa kwa wanaume kila mwaka tangu 1956 wakati Stanley Matthews aliposhinda.

Lewandowski mwenye umri wa miaka 33 aliweka rekodi mpya ya kufunga kwa msimu mmoja katika Bundesliga akiwa na mabao 41 moja zaidi ya nyota wa zamani wa Ujerumani Gerd Müller alipofunga katika dakika ya mwisho katika mchezo uliopita.