Wanadiplomasia wakuu wa Russia na Marekani, Sergey Lavrov, na Antony Blinken, walirushiana maneno Alhamisi, katika mkutano wa kimataifa wa usalama kuhusu vita vya Moscow vya karibu miaka mitatu na Ukraine, wote wakilaumu mataifa yao kuongeza mgogoro.
Lavrov, waziri wa mambo ya nje wa Russia, ameshutumu mataifa ya magharibi kwa kuirejesha vita baridi kwa kusambaza silaha kwenda vikosi vya Kyiv, na kuichokoza Russia, jambo linaloweza kuleta madhara makubwa.
Katika ziara yake ya kwanza ya Umoja wa Ulaya, toka kuanza vita kamili vya uvamizi wa Ukraine, Febuari 2022, pia ameishutumu Washington kwa mazoezi ya kijeshi katika ukanda wa Asia na Pacific ambayo amedai yanalengo ya kuondoa uthabiti wa eneo la mashariki mwa bara la Ulaya.
Aliondoka mkutanoni kabla ya kusubiri kusikiliza majibu ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken.