Maelfu ya raia wa Kuwait wamepiga kura hii leo kuwachagua wabunge, ikiwa ni mara ya pili kupiga kura katika mda wa miaka miwili.
Kuna wagombea 367, wakiwemo wanawake 27 wanaogombania viti 50 vya bunge la taifa.
Mwana mfalme mrithi wa Kuwait alivunja bunge la nchi hiyo mwezi June na kuitisha uchaguzi wa mapema katika hatua ya kupunguza mgogoro serikalini kutokana na upinzani mkali ndani ya serikali ambao ulipelekea shughuli za serikali katika nchi hiyo ndogo kukwama kwa miezi kadhaa.
Wapiga kura wameeleza matumaini ya kupatikana mabadiliko ya kisiasa kati ya serikali na bunge na kuleta hali ya kuelewana ili kuepusha migogoro.
Wagombea wa kike wana matumaini ya kushinda viti kadhaa. Kulikuwa na wagombea wanawake 28 katika uchaguzi uliopita. Hakuna aliyehsinda nafasi yoyote.