Wachunguzi wanaamini uvamizi wa wiki iliyopita kwa watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi nchini Burkina Faso, ulisababisha kutekwa kwa takriban wanawake 60, wasichana na watoto, mwendesha mashtaka wa eneo alisema Alhamisi.
Ripoti za awali zilidokeza kuwa karibu wanawake 50 wamechukuliwa, ilisema taarifa kutoka kwa mwendesha mashtaka wa mkoa wa kaskazini mwa Djibo, Issouf Ouedraogo.
Lakini polisi sasa wanaamini kuwa wasichana na watoto wachanga walikuwa ni miongoni mwa waliotekwa, aliongeza kusema wakati akitangaza kufunguliwa kwa uchunguzi mpya.
Siku ya Jumatano, Vuguvugu la Haki za Kibinadamu la Burkina Faso, lilisema limeandaa orodha isiyo kamili ya wanawake 61 ambao walidai kutekwa, ambayo ilijumuisha takriban 26 ambao walikuwa na umri wa chini ya miaka 18.