Kura zimeanza kuhesabiwa Afrika kusini

Uchaguzi mkuu Afrika kusini, May 8, 2019.

Chama tawala cha ANC kinachotawala tangu uhuru wa nchi hiyo 1994 kinatarajiwa kupata ushindi lakini kinabanwa mwaka huu kutokana na kashfa za rushwa, ahadi zisizotekelezwa na uchumi unaodorora.

Kura zinahesabiwa nchini Afrika kusini kutoka uchaguzi mkuu wa bunge la taifa na mabunge ya majimbo nchini humo baada ya mamilioni ya watu kujitokeza kupiga kura siku ya Jumatano.

Chama tawala cha African National Congress-ANC ambacho kipo madarakani tangu uhuru wa nchi hiyo mwaka 1994 kinatarajiwa kupata ushindi lakini kinabanwa zaidi mwaka huu kutokana na kashfa za rushwa, ahadi zisizotekelezwa na uchumi unaodorora.

Hata hivyo uchaguzi huo wa bunge la taifa na mabunge ya majimbo 9 unasemekana umekuwa na ushindani mkubwa na inaripotiwa kulikuwepo na watu wengi waliojitokeza wakati wa jioni siku ya Jumatano kupiga kura licha ya kwamba wengi walisema hawatashiriki kwenye zoezi hilo la upigaji kura.

Maafisa wa tume ya uchaguzi Afrika kusini walisema huwenda matokeo rasmi yakatangazwa ifikapo Jumamosi.