Serikali ya mkoa mkubwa sana nchini Ethiopia, Oromiya, siku ya Jumamosi ililishutumu kundi la waasi la Oromo Liberation Army (OLA) kwa kuua raia wengi katika mashambulizi yaliyofuatia kushindwa kwa mazungumzo ya amani nchini Tanzania.
Takriban watu 36 waliuwawa wakati washambuliaji wasiojulikana waliposhambulia vijiji vitatu katika wilaya ya Shirka huko Oromiya Novemba 24 na 27, wakaazi waliiambia Reuters.
Hailu Adugna, msemaji wa mkoa wa Oromiya, alilaumu mashambulizi kwa OLA, kundi lililopigwa marufuku la chama cha zamani cha upinzani ambacho kilirejea kutoka uhamishoni mwaka 2018.
Hakuna maoni ya mara moja kutoka kundi la OLA. Msemaji wa serikali ya shirikisho Legesse Tulu hakujibu ombi la kutoa maoni yake.