Kundi ndogo nchini Somalia lenye mahusiano na lile kigaidi la Islamic State linazidi kuwa kubwa, kutokana na kile Umoja wa Mataifa unakielezea kama miminiko ya wapiganaji wa kigeni.
Ripoti mpya wiki hii ya Timu ya Ufuatiliaji wa Vikwazo ya Umoja wa Mataifa kwa Somalia inaonya kwamba wapiganaji, wakiwemo baadhi ya nchi za Mashariki ya Kati, wamesaidia kundi lenye uhusiano na Islamic State, linalojulikana kama IS-Somalia, kuwa na ukubwa wa zaidi ya mara mbili na kufikia kati ya wapiganaji 600 na 700.
“Wapiganaji wa kigeni wanawasili Puntland, Somalia, kwa kutumia njia za baharini na nchi kavu,” kwa mujibu wa ripoti hiyo, ambayo inategemea makadirio ya kijasusi kutoka kwa nchi wanachama wa U.N.
Wapiganaji hao wa kigeni wamepanua na kuimarisha uwezo wa kundi hilo, imeeleza ripoti hiyo, na kuimarisha uwepo wa IS katika eneo la Puntland, Somalia.