Kundi la Hamas limesema wanajeshi wake walimuua mateka mmoja wa Israel na kujeruhi wengine wawili, huku White House ikionya Jumatatu kwamba shambulizi la Iran dhidi ya Israel linaweza kufanyika muda wowote.
Msemaji wa wanamgambo wa Hamas, Abu Obaida ameituhumu Israel kumuua mlinzi wa mateka hao. Alisema mateka wawili wanawake wa Israel walijeruhiwa katika tukio tofauti.
Taarifa hiyo inajiri huku msemaji wa White House anayehusika na masuala ya usalama wa taifa John Kirby akionya kwamba Israel na washirika wake wanapaswa kujiandaa kukabiliana na “ na msururu wa mashambulizi yanayoweza kuwa makubwa” kutoka nchini Iran mara tu “wiki hii.”
Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin Jumapili aliamuru kupelekwa huko Mashariki ya Kati, kwa meli ya kijeshi ya kurusha makombora inayosafiri chini ya maji, USS Georgia, na kuitaka meli ya kubeba ndege za kivita USS Abraham Lincoln kuharakia kuelekea eneo hilo.