Wanamgambo wa Hamas walijipenyeza pia ndani eneo la Israel.
Jeshi la Israel limesema baada ya shambulio la mapema Jumamosi ” Jeshi la ulinzi la Israel litawalinda raia wa Israel."
Waziri mkuu Benjamin Netanyahu amesema Hamas itawajibishwa vikali kwa vitendo vyake.
Gazeti la Israel la Haaretz limeripoti kuwa wanamgambo wa Palestina kutoka Gaza wanawashikilia mateka raia.
Wizara ya afya ya Palestina inasema watu 198 wameuawa katika ukanda wa Gaza katika mashambulizi ya kulipiza kisasi ya jeshi la Israel, na wengine zaidi ya 1,600 kujeruhiwa.
Mamlaka za Israel zimewaonya wakazi katika maeneo karibu na ukanda wa Gaza unaodhibitiwa na Hamas kubaki ndani ya nyumba zao baada ya jeshi la Israel kuonya kwamba “magaidi kadhaa walijipenyeza ndani ya eneo la Israel kutoka ukanda wa Gaza.”
Marekani imelaani shambulio hilo na kutoa rambimbi zake kwa Israel.